Luke 3:10-14

10 aUle umati wa watu ukamuuliza, “Inatupasa tufanyeje basi?”

11 bYahya akawaambia, “Aliye na kanzu mbili amgawie asiye nayo, naye aliye na chakula na afanye vivyo hivyo.”

12 cWatoza ushuru nao wakaja ili wabatizwe, wakamuuliza, “Bwana na sisi inatupasa tufanyeje?”

13 dAkawaambia, “Msichukue zaidi ya kiwango mlichopangiwa.”

14 eAskari nao wakamuuliza, “Je, nasi inatupasa tufanye nini?”

Akawaambia, “Msimdhulumu mtu wala msimshtaki mtu kwa uongo, bali mridhike na mishahara yenu.”

Copyright information for SwhKC